RAHIMU1993.TK.COM

RAHIMU1993.TK.COM
facebook page yetu SKYREPORTS.COM
Sunday, 24 August 2014

07:46

Wanamgambo wateka uwanja wa ndege wa Tripoli


Muungano wa wanamgambo wa Libya umesema kuwa umeteka nyara uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli baada ya siku 10 za mapigano na makundi yanayounga mkono serikali. Kundi la Fajru Libya (Alfajiri ya Libya) limetangaza kuwa limeuteka kikamilifu uwanja huo wa ndege, na kama madai hayo ni kweli itakuwa pigo kubwa kwa vikosi vya wapiganaji kutoka mji wa Zintan vilivyokuwa vikidhibiti uwanja huo tangu kuanguka utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011.
  Wakati huo huo Bunge la Libya limetangaza kuwa makundi ya wanamgambo ya Fajr na Answarul Sharia ni ya kigaidi na limeunga mkono jeshi la nchi hiyo katika kukabiliana na makundi hayo. Tamko hilo limetolewa  asubuhi ya leo ambapo pia Bunge la Libya limekosoea matamshi ya viongozi wa wanamgambo wa Fajr na pia Bunge la Wanamapinduzi wa Benghazi kwamba Bunge la Libya si halali. Limesisitiza kuwa suala hilo ni ishara ya kufanywa mapinduzi dhidi ya taasisi hiyo iliyochaguliwa kisheria na kuendelea vita dhidi ya taifa la Libya.


0 comments:

Post a Comment